Skip available courses

Available courses

 • Kutokana na ongezekola orodha ya ndugu vijana (katika kweli) wa kike na wakiume nchini Tanzania imebainika (imeonekana wazi) kwamba wanahitaji mwongozo. Kila andiko linapumzi ya mungu linaweza kutuhekimisha katika wokovu, ndivyo alivyo andika mtume. Kuna wengi wanaopenda kufundisha lakini, hadi sasa, kuna wachache walio na ufahamu kumaliza kazi hii. Kwa msaada wa masomo haya inatumainiwa kwamba ufundishaji unaweza kuanza na kwamba ndugu zetu wa naume na wanawake na wataanza kukua katika maarifa na imani.

  Kozi hii yenye hatua Nne za mafundisho ya Biblia imetayarishwa kutuchukuwa kikamilifu katika ukweli wote wa maandiko. Kila moja ya hatua tatu za mwanzo ina masomo mia moja na ishirini na tano, yameundwa kwa kukusanya pamoja na vidokezo vya maana vya Historia ya Biblia inavyotiririka na kujifunua. Hatua ya nne ina masomo 1189 kila moja likifungamana na sura yote ya Biblia.

  HATUA YA KWANZA: UTANGULIZI

  Hatua hii ya kwanza imegawanyika katika sehemu tano. Maelezo haya ni sehemu ya tano katika mlolongo (mtiririko) huu wa sehemu ya tano zinazoshughulikia somo kuu la “Ufalme wa Mungu”.

  Masomo yamechaguliwa ili tujifunze kweli ambazo  alifundisha Yesu na ili kwamba tupate tamaa ya kutafuta mengi zaidi yahusuyo Ufalme wa Mungu hatimaye na jinsi/ tutakavyoweza kupata nafasi katika Ufalme ule.

  Wanafunzi wanatiwa Moyo kusoma masomo haya kwa uangalifu na kuwauliza Walimu (Wakufunzi) wao na Wanachama (waumini) wengine kwenye cclesia yao (Usharika wao) kuhusu mambo yaliyozungumziwa katika hadithi zihusikanazo.

  Wakufunzi (Walimu) wanakumbushwa juu ya umuhimu wa kukazia mihimili iliyoainishwa na kuchagua au kupanua maelezo  kadri wanavyoona mahitaji ya mwanafunzi wao mhusika.

  Maswali yamekusudiwa kuchukua masomo makubwa katika kila hadithi.

  Guest access

Skip Navigation

Navigation

Skip Calendar

Calendar

Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat
1 2 3 4 5 6 7
8 9 10 11 12 13 14
15 16 17 18 19 20 21
22 23 24 25 26 27 28
29 30